Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS ATETA NA UJUMBE WA SHIMUTA MJINI DODODMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis Mkanachi ambaye aliongozana na Uongozi na Wajumbe wa Shirikisho kukutana na Makamu wa Rais kwenye makazi yake, Kilimani mjini Dodoma.
********************************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika  ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.Akizungumza baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis Mkanachi alisema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.Pamoja na kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirikisho la Michezo la Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye makazi yake Kilimani, mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.