Habari za Punde

MICHUANO YA TULIA CUP YAANZA KUTIMUA VUMBI KATA YA KIBAMBA

Mshambuliaji wa timu ya Kibamba Worious Emmanyel Athanas (kushoto) akijitahidi kumtoka beki wa timu ya Mpakani FC, Haruna Ramadhani, timu hizo zilipopambana katika mechi ya fungua dimba ya Tulia Cup, katika uwanja wa Kibwegele, Kibamba Dar es Salaam, juzi.
Katibu wa Kamati ya Uratibu wa Michuano ya Tulia Cup Moreen Ngasala akimkaribuisha Diwani wa Kata ya Kibamba (CHADEMA) Ernest Mgawe (kulia) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mpiga wa Kibwegele, katika ufunguzi wa michuano hiyo 
Msanii wa kujitegemea akichangamsha Uwanja kabla ya michuano hiyo kuanza 
Kibamba Warious na Mpakani FC wakiwa tayari kwa mtanange 
MC akitangaza hatua mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi wa michuano hiyo 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Majige aakisalimiana Katibi wa Siasa na Uenezi Kata ya Kibamba Clement Mgabo walipokutana kwenye uzinduzi wa michuano hiyo. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Wadau wa friends Of Tulia wakiwa kwenye michuano hiyo
Mgeni rasmi akienda kukagua timu ili mpambano uanze 
Mgeni Rasmi akisalimiana na mwamuzi wa mechi hiyo 
Mgeni rasmi akisalimia wachezaji wa timu ya Kibamba Warious
Mgeni rasmi akiwa na baadhi ya viongzi baada ya kukagua timu 
Timu zikiwa tayari kwa mpambano
Mmoja wa waraibu wa michuano hiyo Moreen akisoma risala 
Mwenyekiti wa Friends of Tulia akizungumza kabla ya mpambano kuanza 
Wadau wa Friends of Tulia wakiwa kwenye michuano hiyo 
Diwani wa Kata ya Kibamba (CHADEMA), Ernest Mgawe akizungumza kabla ya kipute kuanza. "Michezo siyo siasa, inasaidia sana kuweka jamii pamoja hasa vijana. Napongeza sana uamuzi wa kuanzisha michuano hii", alisema. 
Mgeni rasmi akizungumza kufungua michuano hiyo ambayo leo kuu ni kuwaweka vijana pamoja na pia kuchangisha vifaa na fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Hondogo katika Kata hiyo ya Kibamba. Mgeni huyo rasmi aliahidi kuchangia mifuko mia moja ya saruji 
Wadau wa Friends Of Tulia 
Baadhi ya wadau wakiwa na wachezaji 
Mdau wa Friends of Tulia akiwa na baadhi ya wachezaji 
Mgeni rasmi akijiandaa kupiga mpira kuanshiria mechi kuanza 
Mgeni rasmi akiwa ameshapiga mpira 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na timu zote 
mpambano ukaanza
"Vipi uuko poa?' mwamuzi akimuuliza mchezaji huku akimpapasa baada ya mchezaji wa timu ya Kibamba Warious baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa Mpakani FC
Kipa wa Mpakani FC akiuangalia mpira wakati ukiingia kimiani kufuatia penati iliyopigwa na mchezaji wa Kibamba Warious kutokana na mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa rafu katika eneo la hatari 
Wakiserebuka
Mdau wa Friends of Tulia akiwa na mmoja wa wasanii waliofika kuhangamsha uzinduzi wa Tulia Cup 
Mwandishi wa Uhuru FM akiwa na mmoja wa wasanii waliofika kutia chachandu michuano hiyo 
mdau wa Friends Of Tulia akijaribu kupigapicha baadhi ya matukio kwenye michuano hiyo 
Wadau wakitazama picha zao katika Blog ya taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM Blog). Picha na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.