Habari za Punde

MWANDISHI WA GAZETI LA UHURU MARIAM MZIWANDA APATA AJALI


 Gari ndogo ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, ikiwa imelaliwa na maroli mawili la mafuta na kontena la mizigo baada ya kutokea ajali katika barabara ya Mandera eneo la TOT jana usiku. Imeelezwa kuwa gari ndoho hiyo ilikuwa ikiendeshwa na mwanahabari Huyo Mariam aliekuwa akitoka Chuo majira ya saa tano usiku ajali ikisababishwa na Roli la Mafuta (kushoto) lililokuwa likiikwepa daladala iliyosimama ghafla mbele yA kisha kuhama njia na kukutana na gari hiyo ndogo,huku Roli la mizigo lililokuwa nyuma ya gari ndogo nalo likijitahidi kutaka kukwepa ajali hiyo ambapo lilijaribu kupanda ukuta na kujikuta likiegemea gari ndogo na kuzuiliwa na roli la mafuta. 
Aidha mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa Dereva, Mariam Mziwanda aliwahi kutolewa ndani ya gari hilo baada ya kufanikiwa kuvunja kioo cha nyuma na kumchomoa akiwa amejeruhiwa na kukimbizwa Hospitali.
 Askari akipima ajali hiyo

Askari akipima ajali

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.