Habari za Punde

PATROBASI KATAMBI AMWAGA MBOGA KILICHOMKIMBIZA CHADEMA

Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM, Patrobasi Katambi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake akieleza sababu zilizomtoa Chadema na kuhamia CCM. Mkutano huo ulifanyika kwenye Hoteli ya Protea Oysterbay Dar es Salaam, leo. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo Katambi amesema kilichomkimbiza Chadema ni ukiritimba, ukabila na ubinafsi na mambo mengine yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wake kinyume na taratibu na Katiba ya chama hicho.
******************************************
MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Patrobas Katambi amesema anaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais ,Dk.John Magufuli katika kusimamia rasilimali za Taifa pamoja na kuleta maendeleo.
Amesema kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli si kosa na kufafanua hata wabunge mbalimbali wa vyama vya upinzani wakimo wa Chadema kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimsifu Rais Ujenzi.
Akizungumza Dar es Salaam leo wakati anazungumzia mambo mbalimbali yanayokwamisha vyama vya siasa vya upinzani kupoteza muelekeo kutokana na tabia ya vyama hivyo kuwa mali ya watu badala ya kuwa taasisi imara kwa maslahi ya wananchi walio wengi.
Patrobas amesema kabla ya kujiunga na CCM alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Bavicha) na kutokana na ubabaishaji aliona akiwa Chadema ameamua kuondoka.
Amefafanua wanasiasa wengi ambao wanaondoka upinzani na kujiunga CCM inatokana na utendaji wa Rais Magufuli katika kuwatumikia Watanzania na wala si kosa kuunga mkono jitihada ambazo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
"Kuunga mkono juhudi za Rais si kosa ,ndio maana binafsi nimeamua kuwa mzalendo kwa kuamua kuwa mkweli pale ambapo Serikali inafanya vema lazima niwe mkweli kwa kusifu na kupongeza bila woga.Hivyo sitaogopa kuunga mkono juhudi hizo.
"Ndio maana hata wabunge wa Chadema akiwamo Halima Mdee na wengine tu wamekuwa walikuwa wanampongeza Dk.Magufuli tena akiwa Waziri wa Ujenzi na baada ya kuwa Rais wanasiasa wa upinzani wameendelea kuunga mkono juhudi za Rais katika kusimamia mambo ya maendeleo na yenye maslahi kwa Watanzania,"amesema Katambi.
Kuhusu vyama vya upinzani nchini, amesema changamoto kubwa iliyopo vyama hivyo vingi vimekuwa kama kampuni za watu kwa ajili ya kufanikisha maslahi yao.Hivyo upinzani upo kwenye wakati mgumu kuendelea hadi pale watakapokubali kuwa katika mfumo wa taasisi imara.
Amesema akiwa Chadema ameshiriki kwenye vikao mbalimbali na yapo ambayo anaweza kuyazungumza kwa maslahi ya Watanzania na mengine yabaki kuwa siri yake kwani hawezi kuyasema.
"Vyama vya upinzani viongozi wake wengi wamekuwa wabinafsi, wanashinda kuheshimu maamuzi ya vikao na badala yake wanakuwa na maamuzi yao wenyewe.Wamekuwa binafsi na wanavitumia vyama hivyo kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Akizungumzia kuhusu mafisadi, Katambi amesema wengi waliokuwa wanatuhumiwa kwa ufisadi wengi wamekimbilia vyama vya upinzani na tangu waanze kutuhumiwa hakuna ambaye amekwenda mahakamani kulalamika.
"Hata Dk.Wilbroard Slaa alindika barua ya kujiuzulu mezani na kuondoka Chadema kwa sababu ya mambo ya ufisadi ambayo yeye aliyapigia kelele lakini baadae yaliingia katika chama hicho kwa kupokea waliokuwa wanatuhumiwa kwa ufisadi,'amesema Katambi.
Ameongeza taarifa alizonazo tena za uhakika kuna wabunge wa Chadema 15 wataonndoka chama hicho kutokana na kutoridhishwa na mwenendo unaofanywa na viongozi wao.

"Kuna wabunge wa Chadema wapo njiani kuondoka na kinachoendelea kuweka mambo yao sawa ikiwa pamoja na maslahi yao.Niwahakikishie huko mbele ya safari kuna wanasiasa wengi wa upinzani wataondoka,"amesema Katambi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.