Habari za Punde

RAIS MSTAAFU MKAPA ACHANGISHA SH.MILIONI 292.6 HARAMBEE YA KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI WA KUDHIBITI UKIMWI

RAIS mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akipokea mfano wa Hundi ya Sh. milioni 100 kutoka kwa Meneja Mahusiano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga, wakati wa hafla ya Harambee kuchangia Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku. Tuzo hiyo ilikuwa ni maalumu baada ya Rais mstaafu Mkapa kukubari kuwa mlezi wa TACAIDS, (kulia) ni Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi Vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama. Katikati ni mratibu wa hafla hiyo, Teddy Mapunda. Katika hafla hiyo jumla ya Sh. milioni 292.6 zilipztikana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Rais Mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake, Meneja wa Huduma kwa wateja wakubwa wa benki ya NBC, Salma Mussa.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akihutubia wakati akiongoza harambee ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana usiku. Katika hafla hiyo jumla ya sh. milioni 292.6 zilipatikana
********************************
Na Amina Kasheba, Dar
 RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa amewataka wadau mbalimbali na wananchi kuendelea kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo nchini ambapo zaidi ya sh.milioni 200 zilipatikana.
Mkapa alitoa ombi hilo wakati akiongoza harambee ya kuchangia mfuko huo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya nje na ndani pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
"Ni wajibu kwa kila mwananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia mfuko huu ili kusaidia mapambano ya Ukimwi hapa nchini na kuwa mapmbano hayo si ya mtu mmoja" alisema Mkapa. 
Katika hatua nyingine Rais Mstaafu Mkapa ameiomba Serikali kuendelea kutenga fedha za Ukimwi katika bajeti zake.
Akizungumza katika harambee hiyo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema kwamba Serikali itaendelea kusimamia Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) katika matumizi ya fedha hizo.
Mhagama alisema asilimia 60 ya fedha hizo zitatumika kununulia madawa, asilimia 25 itatumika katika kutoa huduma za kinga pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi na asilimia 15 zitatumika kwa ajili ya uwezeshaji na ufuatiliaji wa programu za Ukimwi.
Mhagama aliongeza kuwa matumizi ya dawa za kufubaza VVU kwa wanawake ni asilimia 92.9 wakati wanaume ni 86.1 na kuwa katika tisini ya tatu kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15-64 ambao wametoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU asilimia 87.7 ya watu hao inaonyesha kiasi cha VVU kimefubazwa wanawake ni asilimia 89.2 na wanaume ni asilimia 84.
Alisema utafiti huo pia umeonyesha kuwa maambukizo mapya ya VVU (HIV incidence) kwa mwaka kwa watu wenye umri wa miaka 15-64 Tanzania Bara ni asilimia 0.29 ambayo ni sawa na watu 81,000.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, Bw. Godfrey Simbeye alisema sekta binafsi imeunga mkono kwa kiasi kikubwa katika kuchangia mfuko huo na kuwa hakutakuwa na matumizi mabaya ya fedha hizo na zitakwenda kutumika kwa kile kilichokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko alimshukuru Rais Mstaafu Mkapa kwa kukubali kushiriki kuongoza harambee hiyo na kueleza kuwa Tacaids imekuwa ikiendesha harambee mbalimbali pamoja na kuandaa mashindano ya michezo na viingilio vyake vimekuwa vikiingia katika mfuko huo.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama akihutubia katika harambee hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akihutubia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi,Bw. Godfrey Simbeye akihutubia.
RAIS mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akipokea zawadi ya Tuzo ktoka kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi Vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama, wakati wa hafla ya Harambee kuchangia Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,juzi usiku. Tuzo hiyo ilikuwa ni maalumu baada ya Rais mstaafu Mkapa kukubari kuwa mlezi wa TACAIDS. 
RAIS mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akimkabidhi cheti Asah Mwambene
RAIS mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akimkabidhi cheti Mwakilishi wa TCRA Mwakyanjala
RAIS mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akimkabidhi cheti Meneja Mahusiano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Benk M wakipokea cheti
Rais mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akimkabidhi cheti Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele
Rais mstaafu wa awamu yatatu, Benjamin Mkapa, akimkabidhi cheti Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa
Mwakilishi wa Montage akipokea cheti
Wadau ndani ya hafla hiyo
Montage wakiendelea kuuza Tisheti...
Mnada ukiendelea....
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akimkabidhi zawadi ya picha Ofisa Uhusiano wa PPF, Lulu Mengela, iliyonunuliwa kwa sh. milioni moja katika harambee hiyo.
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa, akisalimiana na kumpongeza Meneja wa Huduma kwa wateja wakubwa wa benki ya NBC, Salma Mussa baada ya kuchangia katika hafla hiyo.
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa, akimkabidhi zawadi ya picha Meneja wa Huduma kwa wateja wakubwa wa benki ya NBC, Salma Mussa baada ya kuinunua picha hiyo kwa Sh. milioni 1,100, 000/=.
Vijana wa Montage wakipita na picha wakati wa mnada wa kunadi picha hizo kwa waalikwa ili kuchangia mfuko huo.
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa, akimkabidhi zawadi ya picha Meneja wa Hoteli ya Serena baada ya kuinunua picha hiyo kwa Sh. milioni 1, 700, 000/=.
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa, akimkabidhi zawadi ya picha Dkt. Leo Zekeng, baada ya kuinunua picha hiyo kwa Sh. milioni 1,600, 000/=.
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa, akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi wa Kampuni ya Caveha wa Enterprises, Catherne Haule, baada ya kuinunua picha hiyo kwa Sh. milioni 1,050, 000/=.
Wadau kutoka benk M wakiwa katika hafla hiyo
Salma Mussa akisalimiana na Rais mstaafu Mkapa
Wadau kutoka TACAIDS katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Mkapa.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre Group cha Ilala Bungoni, wakitoa burudani wakati wa hafla ya Harambee kuchangia Mfuko wa udhamini wakudhibiti Ukimwi, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Wakibadilishana mawazo
Wadau katika hafla hiyo....
Meza kuu....
Vijana wa Montage wakiuza Tisheti kwa wadau ukumbini hapo
Picha ikinadiwa......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.