Habari za Punde

RWANDAIR YAMPIGA TAFU MWANAMITINDO HASSANALI KUTUA KWA MALKIA WA UINGEREZA

Na Mwanaheri Masoud, Dar
Nguli wa mitindo barani Afrika ,Mustafa Hassanali amealikwa katika hekalu la Buckingham Februar 19 mwaka huu kwa  shughuli ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola.
Hassanali atakuwa ni miongoni mwa wageni wabunifu wengine wa Kimataifa walioalikwa kimataifa kutoka nchi mbalimbali, huku wakisherehekea shughuli ya kifahari inayohusu mitindo ,katika hekalu la malkia wa Uingereza queen Elizabeth, na kufurahia ubora wa kazi za ubunifu.
“Ni heshima kubwa na ufahari kupata mwaliko huu kutoka kwa Malkia ili kuhudhuria sherehe ya kazi za mitindo kutoka nchi zote za jumuiya ya madola ,hii inaonyesha kuwa kazi zangu zinatambulika kitaifa na kimataifa na kujitolea katika sekta ya mitindo ya Tanzania inakubaliwa na kutambuliwa’’ amesema Hassanali
Katika safari hiyo mwanamitindo huyo amepata udhamini katika Shirika la Ndege la Rwanda ambapo atasafiri kutoka Afrika hadi mji wa Gatwick nchini Uingereza kupitia ndege yao ya moja kwa moja A330-300.
“Ni heshima kubwa na tunajivunia kuweza kumsafirisha nguli wa mitindo Mustafa Hassanali aweze kuhudhuria sherehe ya mitindo iliyoandaliwa kwa nchi za jumuiya ya madola.”amesema Meneja wa Rwanda Air nchini Tanzania , Ibrahim Bukenya .

Katika hafla hiyo ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola, inatarajiwa kuhudhuriwa na wabunifu 52 na wataalam wa sanaa za mikono kutoka nchi tofauti za jumuiya ya madola , ambao wataungana kutengeneza nguo moja ya kipekee na endelevu ,ambayo itaonyeshwa kwenye sherehe hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.