Habari za Punde

SHEIKH ALHAD MUSSA AMFUNGUKIA MANGE KIMAMBI


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Al Had Mussa Salumu, amfungukia mwanadada mkosoaji wa mtandaoni, Mange Kimambi, baada ya mwanadada huyo kuandika katika mtandao wake kuwa Sheikh Alhad amekuwa akijihusisha na siasa kwa kukipigia kampeni Chama cha Mapinduzi katika kampeni za uchaguzi zinazoendelea.
Alhad amefunguka kuwa kutokana na mwanadada huyo kuzusha habari asizojua ukweli wake na kusambaza mitandaoni, basi atakuwa amefikia ukomo wa maisha yake na kujisusa na ndiyo maana amenza kuwaandama hata viongozi wa dini.
Aliandika kuwa ''huu ndiyo mwaka wake wa mwisho kutumia mikono pamoja na ulimi wake kutukana watu'', ameandika
Sheikh huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa dini atarudi kupiga goti na kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina rushwa.
Kauli hiyo ya Sheikh Mkuu imekuja ikiwa ni siku moja tutangu picha yake ianze kusambaa mitandaoni na kuanza kutuhumiwa kuwa anashiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi.
"Tutarejea katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina rushwa na tutamuuliza Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia kimya,
.Tunamuonya acheze na namba nyingine lakini siyo viongozi wa dini kwani wao wana mahakama ya kushitakia. Huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kutumia ulimi au mikono yake kudhalilisha watu".
Hata hivyo Sheikh huyo amesema kwamba wapo watu wengi waliompa rai ya kutomjibu Mange Kimambi na kwamba kumjibu kwake kutamfanya atukanwe sana laki amesema kwamba mwanadada huyo aendelee kutukana kwani dua ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi na kama anaishi hapa duniani basi afahamu kwamba hataendelea kuwa salama na amejihalalishia mwenyewe kwa ulimi wake na mikono yake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.