Habari za Punde

TAASISI YA MOYO YA (JKCI) YATOA MAFUNZO YA AFYA YA MOYO NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA WABUNGE MJINI DODOMA

 Mbunge wa Lupa Mhe. Victor Mwambalaswa akiwasisitiza wabunge wenzake umuhimu wa kupima afya zao hasa tezi dume kwa wanaume wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
  Mbunge wa  Bunda mjini  Mhe. Ester Bulaya akieleza jinsi anavyoridhishwa  na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na JKCI ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea mpango wa Serikali kupitia Hospitali za mikoa wa kusomesha madaktari bingwa wengi ili kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalam  hao wakati wa  semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Daktari wa Bunge Jeminian Temba mara baada ya kumalizika kwa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Yona Gandye.
 Wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akielezea kuhusu dalili za shinikizo la damu na tiba yake wakati wa  semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. 
Wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akielezea kuhusu dalili za shinikizo la damu na tiba yake wakati wa  semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Picha na JKCI
****************************
Na Mwandishi wetu, Dodoma
08/02/2018 Wazazi  wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo zote zinazotakiwa ili waweze kuepukana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo.
Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wabunge waliohudhuria semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Waziri Ummy aliwaomba wabunge hao kila wanapokutana na wananchi kupitia mikutano ya hadhara  wawasisitize umuhimu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo cha afya ili wakapate chanjo zinazohitajika kwa wakati.
Aidha Waziri huyo alisema kuwa  matibabu ya moyo pamoja na magonjwa mengine yasiyoambukiza ni ya gharama kubwa na kuwaomba wabunge hao kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao utawasaidia kupata matibabu katika Hospitali zote nchini  ikiwemo JKCI na  Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine Mhe. Ummy aliwataka wakurugenzi wa Taasisi zingine kuiga mfano wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed ambaye kupitia uongozi wake na jitihada zake binafsi Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma bora na kuwahudumia wananchi vizuri katika  matibabu ya moyo na hivyo kuokoa maisha ya watanzania wengi.
“Katika utendaji kazi wa Taasisi hii tunaona juhudi binafsi za kiongozi ambaye kwa jitihada zake  amewatumia marafiki aliosoma nao  na kufanya nao kazi katika nchi mbalimbali kuja nchini kutoa mafunzo kwa wataalam wetu na huduma za matibabu magumu ya moyo ambayo sisi peke yetu tusingeweza kuyafanya kutokana na uchanga tulionao”, alisema Waziri Ummy .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba aliomba katika kikao cha Bunge la Bajeti wabunge wapewe  semina kama hiyo ambayo itaenda sambamba na upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo,  saratani za matiti na shingo ya kizazi, tezi dume na  kisukari.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi aliwasisitiza  wabunge  kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kama watakutwa na matatizo waweze kupata matibabu kwa wakati, kufanya mazoezi na kuepuka kula vyakula ambavyo vitawaepusha kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Katika semina hiyo ya siku moja mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na  Shinikizo la damu na dalili zake na tiba , kiharusi, tezi dume na wanawake  kukoma kwa hedhi kwa wanawake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.