Habari za Punde

WALIOTOSWA KUTAFUNA BILIONI 400 ZA JPM WAHAHA

Mambo mazito yameibuka yakilihisisha gazeti moja la kila wiki kuhongwa mamilioni ya pesa ili kuichafua serikali wakiituhumu kwa tuhuma za uongo kuhusiana na mradi wa hati za kusafiria na uhamiaji kwa ujumla.
Hivi karibuni Gazeti hili liliripoti kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, alizindua rasmi mfumo mpya wa upatikanaji wa hati za kusafiria katika hafla iliyofanyika makao makuu mwa jeshi la uhamiaji kurasini jijini Dar es Salaam huku akiibua siri ya kutaka kutafunwa kwa mabilioni ya shilingi katika mchakato wa utekelezaji wa mradi huo.
Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kitaifa na viongozi wastaafu, Rais pia alitumia hadhira hiyo kulipongeza jeshi hilo la uhamiaji kwa maboresho makubwa hasa kwenye Nyanja ambazo hapo awali palikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea idara hiyo muhimu kuonekana kupoteza heshima mbele ya jamii ya ndani na ile ya kimataifa kiasi cha kupelekea kushindwa kukamata wahamiaji haramu, kushindwa kudhibiti hati za kusafiria mpaka kumilikiwa na watu wasio watanzania, kuichafua hati ya kusafiria kiasi cha kupelekea watanzania kusimamishwa na kucheleweshwa ikibidi kuzuiwa kuingia pindi wasafiripo kwenda nchi nyingine sambamba na vitendo vya rushwa iliyoonekana kukithiri katika idara hiyo siku za awali.
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Nchini Tanzania, Dkt. A nna Makakala
***********************************
‘’unakuta muhamiaji haramu amesafiri kutoka huko akapita chato, kagera, mwanza mpaka anakuja kukamatiwa Singida, utafikiri huko alikopita hakukuwa na maafisa wa uhamiaji, kamishna tafadhali akikamatwa mtu wa aina hii, shughulikia nidhamu ya wakuu wa uhamiaji wa mikoa alipopita mtu hiyo ikibidi hata kuwapunguzia vyeo na nyota zao’’. Alisema Rais Magufuli
Rais aliongeza kuwa hati za kusafiria ni kitu muhimu sana kwa nchi yoyote ile na kile mwenye haki ya kuipata anatakiwa kufuata wajibu wake kuhakikisha anaipata ili imuwezeshe kusafiri nje ya nchi na kwamba hati hizi za kisasa zitakuwa zinapatikana kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini tu (150,000/=) gharama ambayo inaonekana ni nafuu kulinganisha na hadhi, uimara ubora na matumizi wa hati hizo na kulinganisha na gharama zinazotozwa katika nchi nyingine zilizoanza kutumia mfumo huo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Akiendelea kuhutubia katika uzinduzi huo Rais amesema kuwa awali wajanja walipanga kuutekeleza mradi huo kwa gharama kubwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 226 ambazo ukizibadili kwa Dola moja sawa na shilingi 2245 mradi huo ungegharimu shilingi za kitanzania bilioni 507 na kwamba baada ya kugundua ujanja huo Rais alivituma vyombo vya dola kufuatilia na kubainika kuwa mradi huo unaweza kutekelezeka kwa gharama nafuu na za kawaida ambapo baadae mradi umeonyesha kutelekezwa kwa dola milioni 57.8 sawa na bilioni 129 za kitanzania na hivyo kuliokolea taifa upotevu ambao ungeweza kujitokeza wa zaidi ya shilingi bilioni 380.
Katika hafla hiyo Rais amemuahidi kamishna mkuu wa uhamiaji nchini Kamishna Anna Peter Makakala kuwa atawapatia idara hiyo shilingi bilioni kumi ili ziwasaidie kurahisha ujenzi wa ofisi yao ya makao makuu mjini Dodoma ofisi ambayo itakuwa na hadhi sawia na idara yenyewe husika.
Aidha Rais Magufuli amewakumbusha watumishi wa idara hiyo kuzingatia weledi, kutokuendekeza rushwa kuwa wazalendo na kuwajiika ili kuhakikisha wanawahudumia watanzania huku wakiendelea kukusanya mapato yatokanayo na huduma wazitoazo na akaonyesha kushangazwa iwapo mapato hayata ongezeka baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo.
Miongoni mwa vitu vilivyomfurahisha Rais Magufuli kwenye utendaji kazi wa idara hiyo muhimu nchini ni pamoja na kuanza kwa ukusanyaji mapato kwa mfumo wa kielektroniki katika makao makuu ya idara hiyo ya Dar es Salaam,mfumo mpya kuhakiki vibali vya ukaaji na kuhamia Dodoma kutekeleza uamuzi wa Serikali kwa vitendo
Taarifa za uhakika zilizonaswa na gazeti hili zinasema kuwa mmoja kati ya mawaziri waandamizi wa serikali iliyopita ndiye aliyeileta kampuni ya kiingereza ya De ra Lue kampuni ambayo ilitaka kupiga dili hilo la kuandaa hati kwa bilioni 500.
Sambamba na hayo
IDARA ya uhamiaji nchini imewataka watanzania kupuuza habari zinazozagaa kuhusu uvumi wa pasipoti mpya kuwa zimechakachuliwa.
Kauli iliyotolewa jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala amesema wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi kila mara juu ya kila jambo linalohusu maendeleo yao na mambo yanayoletea ustawi wa Taifa letu,sisi ndio wenye taarifa sahihi zinazohusu Mchakato mzima wa Pasipoti Mpya za Kielektroniki
Hivi karibuni Rais Dkt. John Magufuli wakati akizindua hati mpya za kusafiria alisema kumekuwapo na wahujumu wa mchakato huo ambao hawakufanikiwa kuiba sh. bilioni 400.Amesema kumekuwapo kwa watu waliozunguka kila kona na kutumia kila njama zote kupiga vita mchakato huo wakidhani watafanikiwa kuhujumu serikali.
Dkt. Anna Makakala amesema hatua hizo za kutoa na kueneza taarifa zisizo sahihi zinawaletea mkanganyiko wananchi na kudhoofisha mawazo na fikra chanya kwa Taifa lao.Amesema ni vyema jamii kutambua kuwa mchakato wa Pasipoti mpya ya kidigitali ni hatua kubwa kwa Taifa hili na si vyema kuutolea Taarifa zisizo sahihi, amewasihi wanahabari kupata taarifa kutoka katika vyanzo sahihi na kuzifikisha kwa walaji ambao ni Wananchi,”
Amesisitiza hatua ya mafanikio ya matumizi ya hati hizo hazitarudi nyuma kwa sababu ya kuwapo na taarifa zisizo sahihi zenye lengo la kupotosha ukweli wa mchakato huo.“Ni vyema jamii kuelewa kazi ya hati hizo ni kulinda usalama wa nchi yetu hivyo Uhamiaji tutaendelea kudhibiti mipaka ya Tanzania na kulinda usalama wa nchi kwa kuwezesha jamii na raia wa kigeni kufuata taratibu katika utokaji,ukaaji na uingiaji wa kila mmoja,” amesema Dkt. Makakala.
Amesema kila nchi yenye kuhitaji maendeleo ni muhimu kutumia hati ya kusafiria ya kielektroniki ili kufikia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.“Mabadiliko ya kidunia katika maendeleo yanatuonyesha wazi kuwa Taifa hili limefikia kuwa na hati za kisayansi na kiteknolojia hivyo katika hati mpya,mtu yeyote hataweza kutumia ujanja au kughushi na kutumika kwa matumizi yasiyo sahihi,” amesema Dkt. Makakala.
Amesema anaamini idara hiyo haitashindwa na wachache wanaokubali kutumika kuhujumu mchakato huo kwa maslahi binafsi kwakuwa kushindwa kwa mchakato huo ni kupunguza hadhi ya usalama wa nchi.
“Pasipoti ndio kitu kinachotuwezesha kudhibiti wanaoingia nchini na kutoka hiki ni kitambulisho cha raia sehemu yoyote duniani wenye Pasipoti za Tanzania ni mabalozi wa Tanzania mfumo huu utawezesha kudhibiti ujanja wote unaotumika kutakuwa na cheap na security features nyingi sifa ya Taifa letu dunia imeharibika lazima kufanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa letu,” amesema.
Dk. Anna alisema kufanikiwa kwa mradi huo wa e-Immigration kwa gharama ya dola za Marekani milioni 57 imekuwa mwiba kwa vigogo walioondolewa Uhamiaji na sasa wanahaha kwa aibu wakidai kwamba gharama iliyotajwa ni kwa ajili ya mradi mradi mmoja tu wa e-Pasipoti.
“Ni wajibu wa kila mtanzania kuwa macho na wale wote wanaotumiwa na mafisadi kwa ajili ya kuichafua serikali kwakuwa imezuia na kupambana na uhujumu uliotaka kujitokeza,” amesema.
Amesema hati hizo zitawezesha waliopotelewa na hati zao kutumia mfumo wa kiteknolojia na kupakua app yake hata katika simu ya mkononi, hivyo kutambulika na kupewa msaada haraka kokote duniani.Amesema hati hiyo inaviwango vyote vya ubora wa kimataifa pia itatumika kama kitambulisho kwa nchi za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.