Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (wapili kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Willium (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa kikao na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
(kushoto) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia
kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam. Picha
na:
Genofeva Matemu - WHUSM
******************************************************
Na: Genofeva Matemu
–WHUSM
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe ameitaka Tanzania kuitendea
haki heshima ya kupewa nafasi ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa FIFA na
CAF hapa nchini unaotarajiwa kufanyiaka kwa siku mbili mwishoni mwa mwezi
Februari.
Waziri Mwakyembe
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari
kuzungumzia ujio wa viongozi wa FIFA na
CAF nchini kwa ajili ya kufanya mkutano hapa nchini ambao wanatarajia kuwasili
nchini na kufanya mkutana wao tarehe 21
hadi tarehe 22 Februari mwaka huu.
Mhe. Mwakyembe amesema
kuwa Seriakali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wameona
ni vyema kukutana kujadili namna ya kupokea ugeni huo mkubwa kwani Tanzania ina sifa ya kupokea
wageni kwa ukarimu wa hali ya juu hivyo kuhakikisha kuwa watakachokifanya wakifanye kwa hadhi na
hali ya juu ya taifa letu bila ya migogoro ya aina yoyote.
“Ugeni unaokuja kwa
kweli ni mkubwa hivyo fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili ugeni huo uamue
tena kwa mara nyingine kuja hapa nchini kufanya vikao vyake na kuitangaza
Tanzania duniani kote” amesema Mhe. Mwakyembe
Naye Waziri wa Habari
Utalii Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali
Juma amesema kuwa hii ni fursa ya aina yake kwetu sisi kwani itatupa nafasi ya
kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo na kuona ni namna gani michezo
inaweza ikasaidia katika kukuza na kuongeza uchumi kupitia utalii.
“Tunaamini kuwa wageni
hao watakua mabalozi wazuri kwa kutuletea watalii kupitia michezo na kuitangaza
nchi katika mataifa mbalimbali” amesema Mhe.
Juma
Ujio wa viongozi wa
FIFA na CAF ni bahati kubwa kwa nchi yetu na unatokana na matokeo chanya ya
utendaji kazi mzuri unaofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kwa kushirikiana na Serikali lakini pia upigaji vita wa masuala ya rushwa na
upangaji wa matokeo wakati wa mechi.
No comments:
Post a Comment