Habari za Punde

AL MASRI WANAFUNGUKA HATA KWAO: OKWI

LICHA ya kuwa na wakati mgumu wa kufuzu katika hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amebainisha kuwa Al Masry wanafungika.
Simba ililazimishawa sare ya mabao 2-2 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Wekundu wa Msimbazi wana wakati mgumu kuhakikisha wanafuzu hatua ya kwanza na kutinga 16 bora ya michuano hiyo.
Hadi sasa timu ya Al Masry ina faida ya mabao mawili ya ugenini kitu kinachoweza kuwasaidia katika mechi ya marudiano ambapo wanatakiwa kupata ushindi au sare ya 1-1 au ya bila kufungana.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Okwi amesema walishindwa kuibuka na ushindi katika mechi hiyo kutokana na kukosa nafasi nyingi za wazi.
Amesema walikuwa na uwezo wa kuifunga Masry kitu ambacho kilichoshindakana ni ukosefu wa umakini katika kutumia nafasi.
Okwi amesema anaamini wanaweza kufanya maajabu watakaporudiana nchini Misri kwa kuwa ameyaona mapungufu ya safu ya ulinzi ya wapinzani wao.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda, amesema Al Masry inafungika kwa kuwa beki yake ya ulinzi ina fanya makosa mara kwa mara.
Amesema ikiwa katika mechi ya marudiano watakuwa makini kwa kutumia uidhaifu wa beki ya Al Masry, wanaweza kuibuka na ushindi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.