Habari za Punde

AMMY NINJE AKABIDHIWA MIKOBA YA UKOCHA NGORONGORO HEROES

Kocha Ammy Ninje ameteuliwa kuwa Kocha wa muda wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes)
Ninje atakiongoza kikosi hicho kwakuwa Kim Poulsen na Oscar Mirambo wamebaki na majukumu na kikosi cha Timu ya Taifa chini ya miaka 16 Serengeti Boys kinachojiandaa na mashindano ya Cecafa yatakayoanza Aprili 1-15,2018 nchini Burundi.
Kocha Ninje atakiongoza kikosi cha Ngorongoro Heroes kuanzia kwenye mechi zake za Kirafiki za Kimataifa dhidi ya Morocco Machi 17,2018,dhidi ya Msumbuji Machi 21,2018 na mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Vijana chini ya miaka 20 dhidi ya DR Congo zote zikichezwa Uwanja wa Taifa.
Mshindi kati ya Tanzania na DR Congo atakwenda kucheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa mwezi Mei.
Awali Ninje alikuwa kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya wakubwa Taifa Stars ambapo pia alikuwa kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyofanyika nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.