Habari za Punde

ASYA IDAROUS APEWA TUZO YA HESHIMA


Na Amina Kasheba 
MWANAMITINDO  maarufu nchini, Asya Idarous amepewa tuzo ya mwamitindo bora.
Tuzo hiyo alipewa marchi 8 mwaka huu na kampuni ya Life Achievement kama mwanamitindo  ambaye anayebuni mavazi mbalimbali na kusaidia vijana katika sekta hiyo.
Asya Idarous alitangaza kustaafu mwenzi uliopita na kubaki kama mshauri katika jukwaa la Lady in Red na kwa wanamitindo mbalimbali.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu jijini Dar es salaam, Asya, alisema amefurahi kupewa tuzo hiyo kwani ni heshima na kutambua kile anachokifanya pamoja na kutoa fursa kwa vijana.
“Nimefurahi sana na napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hii na wale wote walioniwezesha mimi kupata tuzo hii, kwani wameona umuhimu katika tasnia ya mitindo,” alisema Asya. 
Hata hivyo asya idarous aliwaomba wanamitindo wawe wabunifu katika kuandaa mavazi haswa nchini kwa lengo la kuitangaza nchi na kukua kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.