Habari za Punde

KAMPUNI YA GRACE PRODUCTION YATOA MSAADA WA MAFUTA NA SABUNI KWA WATU WENYE UALBINO (W) ILALA

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Grace Production, Dkt. Elizabeth Kilili, akimkabidhi mafuta na sabuni za kumsaidia kuimarisha ngozi, Fadhila Yusuph (45) wakati mkurugenzi huyo alipokutana na watu hao wenye Ualbino wa Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam. 
 Katibu Mtendaji wa Kata ya Ilala,Terewael Foya akizungumza wakati wa makabidhiano hayo. 
Na Asnath Mkilamwene, Dar
 WATU wenye ualbino katika wilaya ya Ilala wamepatiwa msaada wa mafuta yatakayowasaidia kukinga ngozi zao na maradhi mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Kata ya Ilala,Terewael Foya alisema alipokea maombi kutoka kampuni ya  Grace Product limited kuhusu kuwasaidia watu hao.
Terewael alisema kwa kutambua umuhimu wa mafuta kwa ngozi za watu wenye ualbino  aliikubalia kampuni hiyo na kuandaa utaratibu wa kuwapata wahuska ili kupatiwa msaada huo.k
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Grace Product limited, Dk. Elizabeth Kilili, alisema  ameguswa kuwasaidia watu hao kutokana na kuwaona jinsi wanavyoteseka juu ya ngozi zao.
" Niliona ni vyema kutengeneza mafuta kwa ajili yao kwani siku moja nilitembelea tasisi ya saratani ya Ocean Road na kuona jinsi wanavyoteseka na ngozi zao zikiwa  zimeathirika na vidonda, niliumia sana sababu iliyo sababisha kufanya hivi," alisema.
Msaada huo nitautoa kwa watu hawa kwa wilaya tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, ambapo tayari nimeshafanya hivyo kwa Wilaya ya Temeke na sasa ni Ilala na nitamalizia Wilaya ya Kinindoni,
" Kumbuka ninafanya hivi nikimuunga mkono Rais wetu Dk.John Magufuli kuhusu kauli ya Tanzania ya Viwanda  na hadi sasa nimeshatoa ajira 50 kwa vijana ," alisema.
Hata hivyo, Katibu wa watu wenye Ualbino, Wilaya ya Ilala, Seif Ulate  alisema katika wilaya hiyo kuna  watu 300 wenye matatizo ya ualbino  na wanatakiwa kupewa msaada juu ya ulinzi wa ngozi zao.
 Katibu wa watu wenye ulemavu wa ngozi, Seif, akizungumza
 Mabalozi wa bidhaa za Zoazoa zinazozalishwa na Kampuni ya Grace Production, Nuruel na Banana Zoro wakiwa katika hafla hiyo.
 Mahojiano
 Balozi wa bidhaa za Grace Production, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Banana Zorro, akimkabidhi Bi. Fatuma Abdul na mtoto wake, Salum Abdi, mafuta na sabuni, wakati wa hafla hiyo.
Nuruel akikabidhi mafuta na sabuni kwa mmoja kati ya watoto wenye ualbino..

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.