Habari za Punde

KAMPUNI YA ROCK-EXPLORER YAHIMIZA UTALII WA NDANI


Na Mwanaheri Masoud, Moshi
KAMPUNI ya Rock-explorer ya mkoani Kilimanjaro, imeamua kuanzisha utalii wa ndani ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt. Hamis Kigwangala.
Kampuni hiyo ya Rock-explorer imeanza jitihada hizo kwa ngazi ya chini ili kuweka uimara zaidi katika sekta ya utalii, ambapo imeanza na kuhamasisha wanafunzi kupenda kufanya utalii wa ndani.
“Tumeamua kuanza na wanafunzi tukiamini kuwa wao watakuwa wajumbe wazuri katika jamii yetu kwani watoto hawana sifa ya kupoteza kumbukumbu, hivyo watakuwa makini na wenye mazoea ya kutembelea hifadhi za ndani na kuchangia pato la Taifa, alisema George Mushi.”meneja wa kampuni hiyo.
Watoto wamekuwa na uelewa wa hali ya juu na tunazidi kuwafundisha kwa vitendo ikiwemo kutembelea hifadhi mbalimbali ili kukuza mabalozi wazuri pindi watakapo kuwa na wengine.
Aidha alisema familia nyingi za kitanzania hazina mazoea ya kutembelea hifadhi zetu kama walivyo wenzetu wa mataifa mbalimbali na kuwaomba wazazi na wadau wengine wawe na utaratibu wa kuwazoesha watoto kutembelea hifadhi za taifa kwani hazipo kwa ajili ya wageni pekeyake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.