Habari za Punde

KAMPUNI YA YARA TANZANIA YASHUSHA BEI YA MBOLEA YAKE YA YARA MILA

 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mbolea ya YARA, Linda Byaba, akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, leo wakati akitangaza punguzo la bei ya mbolea hiyo ili kuwapa unafuu wakulima katika kumudu kununua mbolea hiyo maalumu kwa kupandia mazao. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
***************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KATIKA kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano, Kampuni ya Mbolea ya YARA imetoa punguzo la bei ya mbolea yake mpya ya 'YARA Mila Otesha' iliyozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana ili kuwapa unafuu wakulima nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa Kapuni hiyo, Linda Byaba amesema, Kampuni hiyo inaunga mkoni kaulimbiu ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda kwa kupunguza bei ya Mbolea hiyo ili wakulima waweze kupata mazao yaliyo bora kwa faida.
''Kama unavyojua kaulimbiu ya Serikali ni Tanzania ya Viwanda, lakini YARA tunasema Viwanda bila mazao ni sawa na bure na ndiyo maana tumeamua kutoa punguzo la bei kwa wakulima ili waweze kutumia mbolea hii na kuzalisha mazao yaliyo bora na kwa wingi''. amesema Byaba
Aidha Byaba amesema mbolea hiyo imeshuka bei kwa asilimia 50 tofauti na awali ili kila mkulima aweze kutumia mbolea hiyo kwa ajili ya kuboresha na kuongeza thamani katika shamba lake.
Linda ameongeza kuwa mbolea ya Yara Mila Otesha ina faida zisizopungua saba katika shamba ikiwe ni pamoja na kutochachusha udongo na kufanya mazao kuwa mengi zaidi.
ambapo pia utumiaji wa mbolea hiyo inasaidia kuimarisha mmea uliopandwa kukua vizuri na kwa wakati na kumsababishia mkulima kupata faida katika shamba lake.
“Tumeunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa kupunguza bei ya mbolea ili kila mkulima wa hapa nchini aweze kutumia mbolea iliyo bora na kwa bei nafuu’alisema Linda
''Katika zao la mpunga mbolea hiyo inasaidia kukuza mpunga kwa haraka na mkulima kupata mchele ulio bora.
“Mbolea hii pia inasaidia kuyeyuka kwa haraka zaidi kwenye udogo na kufanya mmea upate virutubisho vyake stahiki kwa muda unaotakiwa “amesema
Pia mbolea hiyo inakirutubisho cha fosfofarasi na ina jumla ya virutubisho saba kulinganisha na mbolea nyingine za kupandia mazao.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Mbolea ya YARA, Linda Byaba, akionyesha Mbolea aina ya YARA iliyo maalumu kwa kupandia mazao, wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, leo akitangaza punguzo la bei ya mbolea hiyo ili kuwapa unafuu wakulima katika kumudu kununua mbolea hiyo.
 Mkutano ukiendelea....
Byaba akionyesha kifuko cha mbolea hiyo...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.