Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS TFF MICHAEL WAMBURA AIJIBU KAMATI YA MAADILI

 Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu TFF, Michael Wambura, akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo  kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Kamati ya Maadili ya TFF jana. Kushoto ni Wakili Emmanuel Muga. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Na Leandra Gabriel, Dar
Makamu mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Michael Wambura ameeleza suala kamati ya maadili ya TFF ni la kimkakati zaidi na si la kisheria.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Wambura amesema kuwa suala hili lilianza miaka 14 iliyopita akiwa raia wa kawaida tuu.
Aidha Wambura ameeleza kuwa tatizo lililopo ni uenyekiti wa TFF, fedha na ajira za TFF hasa nafasi ya Katibu mkuu.
Pia Wambura amesema kua kama makamu mwenyekiti wa TFF ataendelea kufanya kazi kama kawaida na lawama hizo zishindwe kabisa, ameongeza kuwa kuna tatizo kubwa sana ndani ya Shirikisho hilo na wananchi watalijua mapema pia ameitaka kamati tendaji kufikiri tena kabla ya kufanya maamuzi.
Naye wakili wa wa     Wambura Emmanuel Muga akiongea na waandishi amesema, kikao hakikufuata sheria hali iliyompelekea kushindwa kufanya kazi yake, amesema barua ya wito ilicheleweshwa na ilipelekwa nyumbani kwake ili hali Wambura yupo TFF. Pia ameeleza kuwa kanuni ya 48 ya maadili ya TFF inayoeleza kuna siku 3 za kuitikia wito haikuzingatiwa na pia kamati haikuzingatia kanuni ya 58 inayoeleza kuhusu kesi na kupanga siku ya kuleta vielelezo na mashahidi haikuzingatiwa kwa mteja wake.
Pia Muga ameeleza kuwa kikao hicho hakikutoa majibu ya moja kwa moja na walieleza watatoa uamuzi siku nyingine.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.