Habari za Punde

MAYANJA AITA 23 KUJIANDAA KUKIPIGA NA CONGO MACHI 22

Na Ripota wa Mmafoto Blog, Dar
BENCHI la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, limetaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachojiandaa na mechi ya kirafiki kati ya Algeria na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo huku ikimteama kiungo, Jonas Mkude.
Tanzania ambayo itachuana na Algeria Machi 22 jijini Alger, itarejea nchini siku moja baadae kwa ajili ya kuchuana na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Machi 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkude ambaye anaitumikia timu ya Simba amekuwa na kiwango kizuri msimu huu ambapo amekuawa akipata nafasi ya kudumu kwenye timu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mara ya mwisho nyota huyo kuitwa kwenye kkosi cha timu ya taifa ilikuwa kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi iliyochezwa Oktoba 7, mwaka jana katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kikosi hicho ambacho kimefanyiwa mabadiliko makubwa na benchi kwa mchezaji Salum Kapombe kurejeshwa kikosini huku idadi kubwa ya wachezaji wa Zanzibar ikiongezeka.
Mara ya mwisho beki huyo kucheza katika kikosi cha timu ya taifa ilikuwa kwenye michuano ya Kombe la COSAFA mapema mwaka jana.
Kwa upande wa Zanzibar, wachezaji walioitwa ni kipa Abdulrahman Mohammed, viungo Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mudathir Yahaya, Abdulaziz Makame na Mohammed Issa ‘Mo Banka’.
Wachezaji wengine katika kikosi hicho ni makipa Aishi Manula, Ramadhani Kabwili.
Mabeki: Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Abdi Banda na Erasto Nyoni.
Viungo: Hamis Abdallah, Said Ndemla, Farid Mussa, Thomas Ulimwengu, Ibrahim Ajibu na Shiza Kichuya.
Washambuliaji: Mbwana Samatta, Saimon Msuva, John Bocco na Yahaya Zayd.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Sueimani ‘Morocco’, alisema wamechagua kikosi hicho kwa kuangalia ubora wa wachezaji.
Alisema kikosi hicho kitaingia kambini Machi 18, mwaka huu ambapo kitasafiri Machi 19 kwenda Algeria kabla ya kucheza mechi hiyo Machi 22, mwaka huu.
Alisema watasafiri kurejea nchini Machi 24, ambapo wataweka kambi ya siku mbili kawa ajili ya kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, machi 27 mwaka huu.
Morocco alisema mechi hizo zitakuwa na umuhimu mkubwa kawa Tanzania kwa kuwa ikiwa watapata matokeo mazuri wanaweza upanda katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Kocha huyo alisema anaamini wachezaji walioitwa wanaweza kuifanya vyema katika kikosi hicho kwa kuwa wengi wao wana uzoefu katika mechi kubwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.