Habari za Punde

NGORONGORO HEROES KUCHEZA NA MOROCCO NA MSUMBIJI, KIKOSI HIKI HAPA


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbuji kabla ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana (AFCON U20).
Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji Jumatano Machi 21, 2018 michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili jijini Kinshansha Congo DR.
Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.

KIKOSI CHA NGORONGORO HEROES KILICHOINGIA KAMBINI HIKI HAPA:-
1.Ramadhan Kabwili(Young Africans)
2.Abutwarib Mshedi(Mtibwa)
3.Johny Kwiyenda(Makongo)
4.Ally Salim (Simba)
5.Kibwana Ally Shomari(Mtibwa)
6.Ally Hussein Msengi(Mbao)
7.Enrick Vitalis Nkosi(African Lyon)
8.Dikson Job(Mtibwa)
9.Assad Juma(Singida United)
10.Said Mussa Bakary(Young Africans)
11.Ally Ng’anzi(Singida United)
12.Kelvin Nashin Naftal(JKT Tanzania)
13.Shaban Ada(Lipuli)
14.Issa makamba(Singida United)
15.Mohamed Rashid(Singida United)
16.Marko Gerald(JMK)
17.Syprian Mtesigwa(Dodoma FC)
18.Muhsin Makame(Njombe Mji)
19.Yohana Mkomola(Young Africans)
20.Ibrahim Abdallah (Miembeni City)
21.Abdul Suleiman(Ndanda)
22.Nickson Kibabage(Njombe Mji)
23.Mussa Najimu(Changanyikeni)
24.Maziku Aman(Makongo)
25.Hamis Mustafa(Ndanda)
26.Samson Myati(Toto Africans)
27.Said Mohamed(Azam FC)
28.Ayoub Mohamed(Young Africans)
29.Mohamed Mussa(Azam FC)
30.Emanuel Myati(Tz Prisons)
31.Riffat Hamis(Mtibwa)
32.Oscar Masai(Azam FC)
33.Paul Peter(Azam FC)
34.Vitalis Mayanga(African Lyon)
35.Rajab Mohamed(Azam FC)
36.Pontia Ohonya
37.Maka Anthony (Young Africans)
38.Israel Mwenda(Alliance)
39.Hance Msonga(Alliance)
40.Moses Kitandu(Simba)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.