Habari za Punde

PAPII KOCHA KUZINDUA 'WAAMBIE' SIKU YA KUZALIWA KWAKE, BUSHOKE,BARNABA KUMPA TAFU


Na Amina Kasheba, Dar
NYOTA wa muziki wa dansi nchini, Johnson Nguza maarufu kama ‘Papii Kocha’ anatarajia kufanya uzinduzi wa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Waambie’ alioutunga mara tu baada ya kutoka Gerezani kwa msamaha wa Rais.
Mwanamuziki huyo Papii na baba yake Nguza Viking, walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha jela ambapo walipata msamaha waRais mnamo Desemba 9, mwaka jana kuachiwa huru.

Uzinduzi huo uliopewa jina la ‘Viking’ unatarajia kufanyika marchi 10 mwaka huu, katika Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo pia kutakuwa na wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya waliothibitisha kumsindikiza Papii, kwa kutambua jitihada zake katika tasnia ya muziki.
Akizingumza na mwandishi wa mtandao huu jijini Dar es salaam, msanii huyo alisema anafuraha kubwa kukutana tena na mashabiki wake na wasanii wenzake katika jukwaa moja siku hiyo na kuongeza kuwa anaamini siku hiyo itakuwa ni ya kipekee zaidi kwa upande.
Aliwataja baadhi ya wasanii waliothibitisha kumsindikiza katika uzinduzi huo kuwa ni pamoja na Barnaba, Bushoke pamoja na baba yake Nguza Viking. 
Uzinduzi huo utafanyika sambaba na sherehe ya kuzaliwa kwake ili kuwa na maana halisi ya mimi kuzaliwa upya na kurudi jukwaani rasmi na uhalisia wa jina la wimbo wangu mpya wa Waambie.
“Nimewamisi sana mashabiki zangu hata wao wamenimisi pia, nilifurahi jinsi walivyonipokea  kilivyopata nafasi ya kuimba japo kwa dakika chache kwenye shoo ya Mapenzi Mubashara ya Aslay na Nandy, hivyo nimeamua kuzindua wimbo wangu mpya wa Waambie Siku tarehe yakuzaliwa kwangu ili nipate fursa ya kufurahi pamoja na mashabiki zabgu”. Amesema
Baada ya uzinduzi huo mashabiki wa muziki wa dansi watarajie vibao vingine vipya kutoka kwa Papii ambavyo tayari amekwishaviandaa ili kuwapa raha Watanzania wote waliommisi katika majukwaa ya burudani. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.