Habari za Punde

TAIFA STARS KUKIPIGA NA ALGERIA NA CONGO MECHI ZA KIRAFIKI

TIMU ya Taifa 'Taifa Stars' inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 – 27, 2018 dhidi ya timu za Taifa za Algeria na DR Congo.
Stars itasafiri kuelekea jijini Algiers kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Algeria Machi 22, 2018 na baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Taifa Stars itarejea nyumbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.