Habari za Punde

TRL YASAINI MKATABA UNUNUZI WA VICHWA 11 VYA TRENI.

Shirika la Reli Nchini TRC limetiliana saini ya makubaliano ya kuvinunua Vichwa 11 vya Treni kutoka Kampuni ya Progress Rail Locomotives ya Marekani ambayo inavimiliki Vichwa hivyo Vyenye namba 9014 hadi 9024.
Mnamo Tarehe 27 September 2017 , Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa aliteua kamati ya wataalamu kwa ajili ya kubaini kama Vichwa hivyo ni vipya au lah.
Mkurugenzi Mkuu wa Shiridka la Reli Nchini Ndugu Masanja Kadogosa amekutana na Vyombo vya habari, na kutoa taarifa hiyo.
 
Masanja amesema kuwa kutokana na makubaliano yaliyofikiwa ya kuvinunua Vichwa hivyo kwa Bei ya Dola za Kimarekani Milioni mbili na laki nne, badala ya Dola Milioni tatu na laki mbili ambazo zilitumika kununua vichwa 13 mwaka 2015, Serikali imeokoa Dola Milioni nane na laki nane.
Masanja Kadogosa-Mkurugenzi Mkuu wa TRC (kushoto) akiwa na Meneja wa Kanda ya Kusini Mwa Jagwa la Sahara wa Kampuni hiyo ya Progress Rail Barend Hanekom, wakionyesha mikataba hiyo 
***************************************
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Kusini Mwa Jagwa la Sahara wa Kampuni hiyo ya Progress Rail Barend Hanekom amesema amefurahishwa kwa mara nyingine tena kufanya baishara na Serikali ya Tanzania.
INSERT-Barend Hanekom-Meneja wa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara
Katika Mkataba huo, imelezwa kuwa itapaswa kufanyika kwa majaribio ya Vichwa hivyo kwa awamu tatu, kwanza ni ukaguzi wa kuvitizama , yaani Visual Inspection , pili ni kuviwasha na kuvipa mzigo lakini vikiwa havitembei yaani Load Box, na tatu ni kufunga na kuvuta mzigo wenye tani 700 kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro na kasha Tani 1200 kutoka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.
Ununuzi wa Vichwa hivi 11 utaongeza ufanisi wa Shirika la Reli kwani sasa hivi Shirika lina Vichwa 29 madhubuti kati ya 47 vinavyohitajika ili kutoa huduma nzuri na uhakika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.