Habari za Punde

UPANGAJI RATIBA ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM WAFANYIKA

Upangaji wa ratiba kwa hatua ya robo fainali na nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam umefanyika leo Ijumaa Machi 2, 2018 kwenye Makao Makuu ya Azam Tv.
Droo hiyo imehusisha timu saba za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na timu moja ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Timu zilizochezeshwa kwenye droo hiyo ni Young Africans,Azam FC,Singida United,Tanzania Prisons,Njombe Mji,Stand United,JKT Tanzania na Mtibwa Sugar.
Mechi za hatua hiyo zitapangiwa tarehe ya kuchezwa baada ya tarehe za awali kuingiliana na mechi za timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 zilizotajwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF.
Ratiba Nane bora
Singida United vs Young Africans          Uwanja wa Namfua
Tanzania Prisons vs JKT Tanzania          Uwanja wa Sokoine
Azam FC vs Mtibwa Sugar                      Azam Complex
Stand United vs Njombe Mji                 Uwanja wa Kambarage
Nusu Fainali
Stand United/Njombe Mji vs Azam FC/Mtibwa
Singida United/Young Africans vs Tanzania Prisons/JKT Tanzania
Fainali

Singida United/Young Africans vs Tanzania Prisons/JKT Tanzania vs Stand United/Njombe Mji vs Azam FC/Mtibwa

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.