Habari za Punde

YANGA NI MWENDO WA KIMYA KIMYA YAICHAPA STAND UTD 3-1

 Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (kushoto) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake bao la tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-1, yaliyofungwa na Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa. Kwa ushindi huo sasa Yanga wanafikisha jumla ya Pointi 46 sawa na watani zao Simba wenye mchezo mmoja mkononi kabla ya kukutana katika mchezo wa Ligi baada ya wote kurejea katika michezo yao ya Kimataifa.
Mchezo wa Yanga na Simba unatarajia kupigwa Aprili 6 
 Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim ajib, mfungaji wa bao la pili akijaribu kumtoka beki wa Stand Utd, Miraji Maka, wakati wamchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
 Winga wa Yanga Yusuph Mhilu, mfungaji wa bao la kwanza akimtoka beki wa Stand Utd, Miraji Maka, wakati wamchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa 
 Mshambuliaji wa yanga Obrey Chirwa akimtoka beki wa Stand Utd, Erick Mulilo na kufunga bao la tatu
Obrey Chirwa, akimtoka beki wa Yanga, Erick Mulilo, wakati wamchezo wa Ligi Kuu Bara  uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa. KWA HABARI KAMILI NA MATUKIO YA PICHA ZA MTANANGE HUU KAA NASI HAPO BAADAYE

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.