Habari za Punde

ABBASI KANDORO AFARIKI DUNIA, KUAGWA MSIKITI WA MANYEMA DAR, KUSAFIRISHWA KWENDA IRINGA KWA MAZIKO

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya, Abbas Kandoro, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibu.
Awali kabla ya kulazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Kandorro alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Aidha Kandoro alistaafu kazi akiwa ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya kabla ya kumwachia Amos Makalla.
 Pia aliwahi kushika nafasi ya ukuu wa mikoa katika zaidi ya mikoa sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Singida na Mbeya. 
Marehemu anaagwa jioni hii katika Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, na kusafirishwa kuelekea Iringa kwa ajili ya maziko.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.