Habari za Punde

ASKARI WA JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN

Kamanda Kikosi cha Tanzania TANZBATT 11 Jimboni Darfur nchini Sudan, Kanali William Sandy kulia akivishwa nishani na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID. Luteni Jenerali Leonard Ngondi katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania Hivi karibuni.
Mnadhimu Mkuu wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID akivisha nishani walinda Amani kutoka Tannzaia katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania hivi karibuni katika eneo la Khor Abeche. (Picha na Luteni Selemani Semunyu)
************************************
Na Luteni Selemani Semunyu
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kikosi cha 11 wametakiwa kujivunia mafanikio yaliyopatikana kufuatia utumishi wao uliotukuka kwa kipindi cha Mwaka Mmoja waliokuwa wakishiriki Ulinzi wa amani Jimboni Darfur nchini Sudan na kutunukiwa Nishani ya umoja wa Mataifa.
Hayo yalibainishwa na mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID jimboni Darfur Luteni Jenerali Leonard Ngondi wakati wa sherehe za kuwatunuku Nishani Askari wa JWTZ katika sherrehe zilizofanyika Khor Abeche na kuhudhuruliwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serkali ya Sudan.
“ Kutunukiwa nishani ni jambo la Kujivunia kwa kuwa zimetolewa kwa sababu Askari wamefanya kazi Nzuri amabayo inapaswa kupongezwa hasa kutokana na Doria zilizofanyika ikiwemo katika safu za Milima ya jaber ambayo inakaliwa na Waasi” Alisema Luteni Jenerali Ngondi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Operesheni ya Jaber Mara Lameck Kawiche alitoa wito kwa Wanajeshi wa Tanzania kuendeleza utayari wao ili kuhakikisha wanalinda heshima ya jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa Weledi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama ilivyotokea Nchini Kongo.
“ Najivunia Utimamu wa jeshi la Tanzania tuna kila sababu kumpongeza Rais na Amiri Jeshi kwa kuridhia Majeshi ya tanznia Kushiki Operesheni za Umoja wa Mataifa sambamba na Mkuu wa Majeshi kya Ulinzi kwa mafunzo kwa Wanajeshi Wake” Alisema Kawiche.
Pia Aliongeza Kuwa Wanjeshi katika utendaji wao wa majukumu katika nchi yeyote ni kielelezo cha nchi husika hivyo Nidhamu na Weledi wa Askari wa JWTZ ni kielelezo cha amani na Fursa zilizopo katika nchi husika .
Kawiche aliwataka Wanajeshi wa Tanzania kutumia Fursa ya kukubalika Kimataifa kuwa kivutio kwa Watalii na wawekezaji lakini kutobweteka na sifa kwani maeneo ya Ulinzi wa amani ni maeneo yanayoweka kubadilika wakati wowote.
Kamanda wa Kikosi hicho ambacho kilifanikiwa kufika katika maeneo amabayo hayakuwahi kufikiwa na Umoja wa Mataifa kmutokan na kukaliwa na waasi na Miundombinu mibovu Kanali William Sandy aliahidi kuendeleza Nidhamu na kusema kauli za Viongozi hai zimezidi kuwapa moyo wa kuafanya kazi kwa umakini ili kutoharibu sifa ya jeshi na nchi kwa ujumla.
Nishani za Umoja wa mataifa kwa Askari polisi na Wanajeshi Walinda Amani zilianza kutolewa mwaka 1950 na kwa Sudan Jimboni Darfur zilianza kutolewa Mwaka 2008.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID Jimboni Darfur Sudan, Luteni Jenerali Leonard Ngondi ( wa Tatu kushoto) akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Khor Abeche katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania Hivi karibuni wa nne Kushoto ni kamanda wa kikosi cha Tanzania Kanali Wiliam Sandy .Picha na Luteni Selemani Semunyu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.