Habari za Punde

KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA DHIDI YA WOLAITTA DICHA, KILA LA KHERI YANGA

KIKOSI cha Yanga kinashuka dimbani jioni hii katika mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika wakiwa ugenini dhidi ya timu ya Wolaytta Dicha ya Ethiopia.
Yanga leo inaingia katika mchezo huo ikiwa na mtaji wa ushindi wa mabao 2-0 walioupata wakiwa nyumbani katika mchezo wa kwanza uliochezwa April 7 mwaka huu.
Katika mchezo wa Kwanza Yanga wakicheza bila nyota wake watatu waliokuwa wakitumikia adhabu ya kadi mbili za njano ambao katika mchezo huo wamejumuishwa kwenye kikosi cha kwanza.
Yanga wakiwa chini ya Kocha msaidizi Noel Mwandila na Shadrack Nsajigwa kitashuka dimban katika uwanja wa Hawasa kutafuta ushindi wa aina yoyote, sare au kutokufungwa goli zaidi ya moja.
Ambapo kwa matokeo hayo yataibeba Yanga na kutinga hatua ya Makundi ya kombe la Shirikisho na kujinyakulia kitita cha sh. milioni 600.

KIKOSI KINACHOANZA LEO
Youthe Rostand
Hassan Ramadhan 
Haji Mwinyi
Abdallah Shaibu 'Ninja'
Kelvin Yondani
Pappy Tshitshimbi
Thabani Kamusoko
Raphael Daud
Pius Buswita
Obrey Chirwa
Yusuf Mhilu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.