Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Mhe. January  Makamba akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
   Waziri wa Katiba na Sheria Prof.  Palamagamba  Kabudi akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mery Mwanjelwa akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wakulima wa Korosho wanapata malipo  yao kwa wakati mara baada yakuuza  zao hilo.
   Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akisisitiza jambo Bungeni mapema leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Job  Ndugai akisisitiza jambo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo.
Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mapema leo Bungeni mjini Dodoma. Picha na Frank Mvungi-  MAELEZO, Dodoma

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.