Habari za Punde

MECHI YA LIPULI VS SIMBA YASOGEZWA MBELE

Mechi namba 202 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Lipuli na Simba iliyopangwa kufanyika Ijumaa, Aprili 20, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa imesogezwa mbele kwa siku moja.
Sasa mechi hiyo itachezwa Jumamosi, Aprili 21, 2018 kwenye uwanja huo huo. Sababu za mabadiliko hayo ni wamiliki wa uwanja kuutumia Aprili 20, 2018 kwa shughuli nyingine za kijamii.
Pia kwa mujibu wa ratiba, Yanga ambayo iko nchini Ethiopia, baada ya kurejea itacheza na Mbeya City mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, Jumapili Apirili 22, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.