Habari za Punde

MFAUME MFAUME ATWAA MKANDA WA AFRIKA MASHARIKI BAADA YA KUMTWANGA HABIB PENGO

 Bondia Mfaume Mfaume kutoka Mabibo, akinyanyua mkanda wake juu wa Ubingwa wa Afrika Mashariki baada ya kumtwanga Habib Pengo katika pambano la raundi 10 lililofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi Sinza jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hamis Lissu, akimvisha Mkanda wa Ubingwa wa Afrika Mashariki, Bondia Mfaume Mfaume, baada ya kumtwanga Habib Pengo katika pambano la raundi 10 usiku wa kuamkia leo.
 Bondia Mfaume Mfaume wa Mabibo (kushoto) akikwepa konde la Habib Pengo, wakati wa pambano la raundi 10 la kuwania Mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki, lililofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi Sinza jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Katika pambano hilo, Mfaume alishinda kwa Pointi na kutwaa mkanda huo.
 Bondia Habib Pengo wa Manzese (kulia) akimtwisha konde zito mpinzani wake Mfaume Mfaume, wakati wa pambano la raundi 10 la kuwania Mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki, lililofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi Sinza jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. 

 Bondia Kanda Kobongo (kushoto) akipambana na Mada Maugo, wakati wa pambano lao la utangulizi la raundi 8. Katika pambano hilo Mada Maugo alishinda kwa pointi.
 Mpambano ukiendelea.......
 Maugo akiwa chini baada ya konde zito......

  Mashabiki wakimbeba bondia Kanda Kabongo wakimshangilia wakidai kuwa ndiye mshindi katika pambanolake na Maugo huku wakisikika wakisema Maugo kapendelewa....
 Bondia Dullah Mbabe aliyegoma kupanda ulingoni akiwa na mtangazaji wa mapambano hayo akielezea sababu za kugoma kupanda ulingoni ambapo alidai kuwa ni suala la kutokupewa pesa za mkataba wake wa kucheza pambano na ama Mwakyembe ama Mbelwa.
 Bondia Lole Japhet (kulia) akichapana na Toni Rashid wakati wa pambano lao la utangulizi la raundi 8. Katika pambano hilo Lole alishinda kwa pointi
 Chukua hiyo..........
Lole akipelekwa chin na kuhesabiwa.......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.