Habari za Punde

RAIS DKT.MAGUFULI KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO UHURU WA HABARI NCHINI

Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane Mahanji akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyokwenda begakwabega na waandishi kwa kuto semina ili kutoa habari zenye faida kwa Taifa.
Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa akizungumza na waandishi wa habari wanavyochangia kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari kwa kutoa pesa ili vyombo hivyo vijiendeshe.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na waandishi wa habari kuhusuumoja wa Mataifa unavyodhamini mchango mkubwa wa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.
********************************************************
RAIS Dkt. John Mgufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru wa habari Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma Mei 2 hadi 3 mwaka huu ikiwa ni kilele chake na kauli mbiu ikisema ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa sheria.
Ambapo wageni zaidi ya 300 wanatajiriwa kuhudhuria hafla hiyo wakiwepo wadau , wanahabari ,wabunge na taasisi mbalimbali ambapo kimataifa Afrika inafanyika Nchini Ghana Accra zaidi ya nchi 100 zitawakilisha katika hafla hiyo.
Akizungumza jjjini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Jangwa la Sahara Salome Kitomari amesema katika siku hizo watazungumzia umuhimu wa uhuru wa habari, utawala bora kwa waandishi wa habari na wanasheria kama Mahakama kuwa na uhuru wa kusimamia kesi za jinai za kuwa na uwazi kwa wanahabari vilevile na kukumbusha kutekeleza majukumu katika uandikaji wa habari kuwa sahihi.
Aidha Makamo wa Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Jane Mihanji amesema wao wamekuwa na jukumu la kuwaweka pamoja waandishi wa habari na kuwapa mafunzo na kuwapatia vitendea kazi.
Ametaja baadhi ya vitendea kazi hivyo ni kamera na kompyuta ili kurahisishia majukumu yao ya kuhabarisha umma ambapo amesisitiza kutokana na uhaba wa vyumba vya habari mikoani inakuwa vigumu kupata stori kutoka nje ya Dr es Salaam.Hivyo amesema wamewajengea uwezo wa mafunzo ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa rafiki katika utendaji.
"Tumeshuhudia stori ikiwa inatoka lakini katika kufufua maovu yanayotendeka inaleta misukosuko, hivyo tunaomba Serikali kuwajibika kufanya kazi yake kwenye upande wa haki na waandishi wa habari kutoa taarifa bila kupendelea mtu na kutoa chukua rushwa,"amesema Mahinja.
Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa amesema watashirikiana na wadau wengine kwenye tasnia ya habari kuadhimisha siku hiyo umuhimu na wapo kwa ajili ya kuimarisha vyombo vya habari vinafanya kazi katika mazingira rafiki na kuhakikisha wanahabari kutoa taarifa makini zenye ubora kwa jamii.
Kwa upande wa Ofisa habari wa Umoja wa Wataifa (UN) Stella Vuzo amesema kwa sasa umoja huo unatekeleza maendeleo endelevu ifika 2030 kila nchi hupaswa kuelezea namna gani imetekeleza hilo lengo na kuhakikisha kuwepo na ushirikiano kwa wanahabari kusaidia kupata taarifa mbali mbali .

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.