Habari za Punde

RC TABORA: VIONGOZI MSIGEUZE USHIRIKA KUWA KICHAKA CHA KUFICHA MAOVU

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua Mkutano wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo jana wilayani Igunga.
Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Pamba ambavyo ni wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 22 uliofanyika mjini Igunga
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo Lazaro Ngullo(kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama hicho uliofanyika mjini Igunga jana.Wengine ni Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri(kushoto) na Mkuu wa Wilaya John Mwaipopo (katikati)
Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Pamba ambavyo ni wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 22 uliofanyika mjini Igunga
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule (kushoto)akitoa ufafanuzi jana kwa viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa wakulima wa Pamba kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo. Wengine ni Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri(katikati) na Mkuu wa Wilaya John Mwaipopo (kulia)
Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo (wa pili kushoto) akichangia mada jana kwenye Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo.Wengine ni Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri(kushoto) Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo Lazaro Ngullo(wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Nzenga Godfrey Ngupula (kulia)
***************************************
NA TIGANYA VINCENT, RS TABORA
SERIKALI imewaonya Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika Mkoani Tabora ambao wanafikiri wanaweza kugeuza Ushirika kuwa maficho ya kuwanyonya wakulima kuondoka mara moja kabla ya hatua kali hazichukuliwa dhidi yao.
Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo.
Alisema kiongozi aliye madarakani ajipime kama ni safi na mwadilifu na sio kuwa kama kibaka mzoefu.
Mwanri aliongeza kuwa watu wanaofanya ujanja ujanja kwa ajili ya kutaka kuwanyonya wakulima wawachukulie hatua mapema kabla ya mambo hajaharibika.
Alisisitiza kuwa kila kiongozi ajifikie moyoni mwake kama kweli anaweza kuwa msafi ndio awe kiongozi.
Aidha Mkuu huyo Mkoa alisema maelekezo ya serikali ni kwamba pamba yote itauzwa kupitia ushirika na sio vinginevyo kwa kuwa lengo ni kutaka mkulima asinyonywe.
Alisema ushirika ndio njia pekee inayokuwa njia pekee ya kuwashika mkono wakulima wanyonge.
Naye Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule alisema kuwa kiongozi yoyote aliyewania uongozi kwa ajili ya maslahi binafsi ni vema ajiondoe mapema katika Ushirika ili asije akajikuta sehemu mbaya.
Alisema kiongozi atakayekutwa akiwa amegeuza Ushirika kama sehemu ya kupatia fedha kinyume cha Sheria atakamatwa na hataachiwa na atashitakiwa kama mhuhujumu uchumi.
Aidha Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule aliwataka viongozi wa Ushirika kutoishia katika kukaa Ofisini bali nao walime pamba ili wakulima wengine waende kujifunza jinsi ya kulima vizuri.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.