Habari za Punde

SERENGETI BOYS YAIFURUSHA KENYA NA KUTINGA FAINALI CECAFA U17

TIMU ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA U17 baada ya leokuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya katika mchezo wa Nusu fainali kwenye Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.
Katika mchezo huo Kenya ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao na kuwafanya Serengeti Boys kufanya kazi ya ziada kutafuta baola kusawazisha na baadaye bao la ushindi.
Mabao ya Serengeti Boys leo yamefungwa na Jaffar Juma dakika ya 21 kipindi cha kwanza na Kelvin Paul dakika ya 62 kipindi cha pili,ambapo sasa Serengeti Boys watakutana na Somalia katika mchezo wa fainali unaotarajia kupigwa siku ya jumapili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.