Habari za Punde

SIMBA YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA, YAWACHEZESHA KWATA MAAFANDE WA TZ PRISONS

 Washambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi (kushoto) na John Bocco, wakishangilia, bao la kwanza lililofungwa na Bocco katika kipindi cha kwanza,wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika hivi punde kwenye kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco katika dakika ya 35 na Emmanuel Okwi katika dakika ya 80. Picha na Muhidin Sufiani,  (MAFOTO).
 Beki wa Simba Shomari Kapombe (kushoto) akiwania mpira na wachezaji wa Tanzania Prisons, Leonsi Mutalemwa (katikati) na Eliuter Mpepo, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 John Bocco (kushoto) akiwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, Leonsi Mutalemwa, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
 Emmanuel Okwi, akijipinda kupiga shuti huku beki wa Tanzania Prisons, Nurdin Chona, akijaribu kuokoa, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Asante Kwasi (katikati) akiwania mpira na mabeki wa Tanzania Prisons, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.