Habari za Punde

UJENZI WA JENGO LA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI DODOMA - TBA YATAKIWA KUONGEZA KASI.


Hili ni Eneo la Maghala ya kuhifadhia vifaa vya Uchaguzi likiwa katika hatua za Ujenzi.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R), Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia) na Wajumbe wa Tume  wakiangalia eneo la linapojengwa jengwa la Utawala la  Tume ya Taifa ya Uchaguzi enero la Njedengwa mkoani Dodoma. Wajumbe wa NEC wametembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Ofisi za NEC mkoani Dodoma.
 Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipokea taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mradi kutoka TBA, Arch. Steven Simba.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R), Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) na Wajumbe wa Tume  wakielekea katika eneo la ujenzi wa Ofisi za Tume mkoani Dodoma. Wengine alioambatana nao ni Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume kutoka Chuo Kikuu Ardhi QS Godwin Maro (kushoto) na Mhandisi Yohana Mashauri - Mhandisi wa Mradi huo kutoka TBA
**********************************************************
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wamefanya ziara ya kutembelea eneo la mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume eneo la Njedengwa mkoani
Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo.
Ujenzi huo unafanywa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) na Kusimamiwa na Chuo Kikuu Ardhi.
Kufuatia ziara hiyo Wajumbe wa NEC wameonesha kutoridhishwa na Kasi ya ujenzi ya Mkandarasi anayejenga ofisi hizo (TBA) na kutoa wito kwa mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.