Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE KUWAPOKEA SERENGETI BOYS ALFAJIRI

TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17(Serengeti Boys) iliyokuwa irudi nchini Jumatano Alfajiri sasa inatarajia kurudi Alfajiri ya kuamkia Jumanne Mei 1,2018.
Mabadiliko hayo yametokana na Baraza la Vyama na Vilabu Africa Mashariki na Kati CECAFA kubadili tiketi za ndege za Serengeti Boys.
\Serengeti Boys wanaotarajia kutua kwa Shirika la Ndege la Rwanda Alfajiri saa 9 watapokewa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.
Serengeti Boys wametwaa ubingwa huo wa Cecafa baada ya kuifunga Somalia katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Ngozi kwa mabao ya EdsonJeremiah na Jaffar Juma Mtoo.
Katika mashindano hayo Serengeti Boys ilitoka sare 1-1 na Uganda kabla ya kuifunga Sudan 6-0 na baadaye kuichapa Kenya kwa mabao 2-1 kwenye nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.