Habari za Punde

YANGA NDO BASI TENA, YALAZIMISHWA SARE NA SINGIDA UTD NYUMBANI

Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu, akiifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 45 plus kipindi cha kwanza wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu (chini) na mshambuliaji Obrey Chirwa wakishangilia bao.
 Kiungo wa Yanga, Raphael Daud (kulia) akiwatoka mabeki wa Singida United, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim AJib (kulia) akichuana kuwania mpira na Kiungo wa Singida United, Deus Kaseke, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga, Yusuph Mhilu, akipiga shuti ndani ya 18 na kukosa bao wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es  Salaam. 
KWA HABARI KAMILI NA MATUKIO YA PICHA ZA MTANANGE HUU KAA NASI HAPO BAADAYE

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.