Habari za Punde

YANGA YAANZA NA 2-0 NYUMBANI DHIDI YA WOLAITTA DICHA SC YA ETHIOPIA

 Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya Raphael Daud (katikati) kuifungia timu yake bao la kwanza katika sekunde ya 39 kipindi cha kwanza dhidi ya Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia, akiunganisha krosi murua ya beki wa kushoto, Haji mwinyi wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Kiungo wa Yanga, Raphael Daud (katikati) akijaribu kuwania mpira na wachezaji Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia beki, Mubarik Shikori na kipa, Wond Wosen Gereman, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano unatarajia kupigwa jumatano ya wiki ijayo Aprili 18 nchini Ethiopia. 
 Yusuph Mhilu, akiruka kupiga kichwa na kukosa bao....
 Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (kulia) akiwa jukwaani akifuatilia mchezo huo akitumikia kadi mbili za njano, ambapo anatarajia kucheza katika mchezo ujao wa marudiano.
Winga wa Yanga, Yusuph Mhilu, akiwatoka mabeki wa Wolaita Dicha SC ya Ethiopia, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Nyota wa mcheo wa leo Yusuph Mhilu akiwahenyesha mabeki wa Wolaitta
 Mwinyi Haji, akiwania mpira na beki wa Wolaita Dicha SC ya Ethiopia, Yared Dawit, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, 
Ibrahim Ajib wa Yanga, akijaribu kuwatoka mabeki wa Wolaita Dicha SC ya Ethiopia, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.