Habari za Punde

YANGA YAVUNA MILIONI 600 ETHIOPIA, YATINGA HATUA YA MAKUNDI 16 BORA

WAWAKILISHI wa Tanzania katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, Yanga leo wametinga hatua ya makundi Barani Afrika na kuvuna kitita cha sh, Milioni 600 baada ya kuwaondosha katika michuano hiyo, Waethiopia timu ya Wolaitta Dicha kwa wastani wa mabao 2-1.
Katika mchezo wa awali uliochezwa jijijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa, Yanga waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0 na kujihifadhia mtaji wa kutangulia hatua moja mbele ya kufuzu michuano hiyo jambo ambalo wamefanikiwa hii leo.
Wolaitta Dicha katika mchezo wa leo walifanikiwa kupata bao la mapema katika dakika ya pili kipindi cha kwanza na kuwaondoa mchezoni Yanga, hadi kipindi cha pili ambapo Yanga walionekana kubadilika na kushambulia zaidi.
Wolaitta pia katika kipindi cha pili walionekana kubadilika na kuanza kupiga mipira mirefu tofauti na kipindi cha kwanza na katika mchezo wa kwanza waliocheza jijini Dar, ambapo walionekana kupiga pasi nyingi fupi fupi na kushambulia kwa kushitukiza.
Yanga wanavuna  mamilioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi 16 bora baada ya ushindi wa leo ambapo ratiba hiyo inatarajiwa kupangwa kesho.
Baada ya ushindi huo Yanga itaipa faida nchi ya Tanzania iwapo itaendelea kufanya vizuri katika hatua hiyo ya makundi ambapo itaipa nchi nafasi ya kuongeza timu katika michuano hiyo kama ilivyo kwa nchi ya Congo na wenzetu wa Misri ambao wana jumla ya timu nne zinazoshiriki michuano ya Kombela la Mabingwa Barani Afrika na Shirikisho.
Lakini pia Yanga watapata fursa ya kusajili wachezaji watatu ili kuongeza nguvu kuelekea hatua hiyo ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.