Habari za Punde

BREAKING NEWS: DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally kwenye meza kuu mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally wapili kutoka kulia kwenye meza kuu kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa NEC hawaonekani pichani, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwashukuru Wajumbe wa NEC kwa kumpitisha kuwa Katibu Mkuu wa Chama Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe mara baada ya kikao cha NEC Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.