Habari za Punde

MAONESHO YA NISHATI MBADALA WA MKAA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TANGAZO
MWALIKO WA KUSHIRIKI MAONESHO YA NISHATI MBADALA WA MKAA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI,
31 MEI -  5 JUNI, 2018, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM
Ofisi ya Makamu wa Rais inawaalika wadau kutoka taasisi za serikali, zisizo za serikali, sekta binafsi, taasisi za utafiti na vyuo vikuu kuonesha bidhaa, ubunifu na uvumbuzi wao katika teknolojia mbalimbali za nishati za kupikia ambazo ni mbadala wa mkaa. Vile vile katika eneo la maonesho wajasiriamali waliowekeza au wenye nia ya kuwekeza katika teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa watapewa elimu ya ujasiriamali kuhusu masuala na fursa mbalimbali katika biashara ya uendelezaji wa nishati mbadala. Pia taasisi za fedha zitatoa taarifa za mikopo kwenye ujasiriamali wa nishati.
Maonesho haya yatafanyika kuanzia tarehe 31 Mei hadi 5 Juni, 2018 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Maonesho haya ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa maadhimisho haya yatafanyika Jijini Dar es Salaam. Aidha kwa sehemu kubwa maonesho haya  yatalenga kuchochea ujasiriamali na biashara na nishati mbadala wa mkaa na kuelimisha na kuhamasisha wananchi wote kuondokana na matumizi ya mkaa ili kuokoa misitu yetu na kuhifadhi mazingira.
Wadau wote wenye teknolojia mbalimbali zinazohusu hifadhi ya mazingira ikiwemo kurejereza (recycling) plastiki pia wanakaribishwa kushiriki.
Kwa kuwa fursa hii ni adhimu na adimu ni vema wadau wanaohitaji kushiriki kujiandikisha mapema iwezekanavyo hadi ifikapo tarehe 20 Mei, 2018. Aidha, kila mshiriki wa maonesho haya atatakiwa kulipia gharama za ushiriki ili kuwezesha ushiriki wake, ikiwemo kusafirisha vifaa vyake. Maombi ya ushiriki yaambatane na maelezo mafupi ya teknolojia ya nishati mbadala itakayooneshwa.
Kwa maelezo na mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na Maafisa wafuatao Ofisi ya Makamu wa Rais:
Ndg. Deogratius Paul, 0769257570;
Ndg. Timotheo Mande, 0745 819 197
Wasilisha maombi ya ushiriki kwa:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Makamu wa Rais,
Barabara ya Makole,Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7,
S. L. P 2502,
40406 DODOMA,
Barua Pepe: km@vpo.go.tz; Simu: +255 026 235 203 8/0769257570

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.