Habari za Punde

MAPOKEZI YA TIMU YA VIJANA YA SERENGETI BOYS KATIKA PICHA

Nahodha wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys Morice Michael akiwa amenyanyua juu kombe la ubingwa wa CECAFA 2018 walilonyakua nchini Burundi baada ya kuwasili Dar es salaam alfajiri ya leo. Serengeti Boys wametwaa ubingwa huo wa Cecafa baada ya kuifunga Somalia katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Ngozi kwa mabao ya EdsonJeremiah na Jaffar Juma Mtoo.Katika mashindano hayo Serengeti Boys ilitoka sare 1-1 na Uganda kabla ya kuifunga Sudan 6-0 na baadaye kuichapa Kenya kwa mabao 2-1 kwenye nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akikabidhiwa na RAis wa TFF kombe la ubingwa wa CECAFA la vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya Serengeti boys kuwasili nalo Dar es salaam
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa na Serengeti Boys na viongozi wao baada ya mabingwa hao wa U-17 CECAFA 2018 kuwasili alfajiri ya leo Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.