Habari za Punde

MGANGA MFAWIDHI KAKONKO AJINYONGA KWA TAULO, DC ASHANGAZWA


Na Rhoda Ezeikel Kigoma,

MGANGA Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kakonko wilayani Kakonko mkoani kigoma Dk.Mejo Banikila ( 43 ) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia taulo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kanali Hosea Ndagala alipokuwa akizungumzia tukio hilo na kwamba wakati alipofika nyumbani kwa marehemu huyo kuangalia tukio hilo ameelezwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo Dk.Banikila alikutuwa amejinyonga.
Kanali Ndagalla amesema matukio ya watu kujinyonga katika wilaya ya Kakonko yamekuwa yakiongezeka na wanaendelea na uchunguzi ili kubaini sababu hasa za watu kuchukua maamzi magumu kama hayo.
Aidha Mkuu huyo amewataka wananchi kuhudhuria Kanisani na misikitini ili kusikiliza mahubiri na kupunguza msongo wa mawazo kwa kuwaeleza wenzao ilikwaweze kuwashauri na kuepukana na tatizo hili la Wananchi kujinyonga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno alithibitisha kutokea tukio hilo na kuwaomba wananchi kuacha kuchukua maamuzi ya kujinyonga kwa sababu yeyote ile kwakuwa ni matukio ambayo yameendelea kutokea nchini na kwamba wanaendelea na uchunguzi kujua sababu iliyosababisha mganga huyo kuchukua uamuzi huo.
Kwa upande wao baadhi ya wapangaji wenzake wamesema kwa muda wa miezi nane wameyo ishi naye wameishi nae vizuri licha ya kuwa siku mbili kabla ya tukio amekuwa akionekana mnyonge mpaka tukio hilo kutokea .
Walisema Mganga huyo alikuwa akifanya kazi zake vizuri na amekuwa akijitoa sana kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma kwa wakati na kwamba watamkumbuka kwa Mambo mengi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.