Habari za Punde

MSANII LULU MICHAEL SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE

Muigizaji Elizabeth Michael, maarufu Lulu leo Jumatatu Mei 14, 2018 amebadilishiwa adhabu na sasa anatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzani, ambapo Magereza imethibitisha kuhusu uamuzi huo.
Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.
Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ambaye baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa upande wa mshtakiwa alitoa hukumu.
Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mpenzi wake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.