Habari za Punde

MSEMAJI WA AZAM FC JAFFAR IDD AWATAKA SIMBA NA WATANZANIA KUISAPOTI YANGA KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA

 Msemaji wa timu ya Azam Fc, Jaffar Idd, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo.
***************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog.Dar
Uongozi wa Azam Fc umewataka watanzania kuwa wazalendo na kuwaombea wawakilishi wa Tanzania Yanga kwenye michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Yanga inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wao kwanza wa kundi D dhidi ya USM Alger utakaofanyika Mei 6.
Akizungumza leo Jijini Dar Es Salaam Ofisa habari wa Azam Fc Jaffar Idd Maganga amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na kuiombea Yanga iweze kufanya vizuri kwenye michuano hiyo kwani ndio wawakilishi pekee wa michezo kimataifa waliosalia.
"Yanga ndio wawakilishi waliosalia kwenye michuano ya kimataifa baada ya Simba kuondolewa katika kombe la Shirikisho ambalo Yanga wanacheza kwa sasa baada ya kuondolewa Klabu Bingwa Afrika," amesema Maganga.
"Kwa sasa hakuna wawakilishi wengine na imekuwa vizuri zaidi tumeona kuwa Yanga imefanikiwa kuingia hatua ua makundi kwahiyo ni moja ya fursa kubwa sana kwanza kuziona timu hizo pia wachezaji wetu watapata fursa ya kujitangaza zaidi kimataifa,"
Maganga amesema kwa sasa ni muda wa kuwa wamoja na wazalendo kuisapoti timu ya Yanga ili waweze kufanya vizuri kwenye michezo yao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.