Habari za Punde

MWILI WA MBUNGE KASUKU BILAGO WAAGWA LEO JIJINI DAR


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umeagwa leo jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameongoza mamia ya waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo, Mbowe amesema mwili wa Bilago utapumzishwa kwenye nyumba yeke ya milele Alhamisi wiki hii mkoani Kigoma na kesho wabunge watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho mkoani Dodoma.
Kuhusu ratiba ya mazishi Mbowe amesema wamekaa kikao na familia na kukubaliana mwili wa marehemu Bilago upumzishwe Almasi ili kutoa nafasi ya wananchi wa jimbo lake kumuaga na kutoa heshima zao za mwisho.Amefafanua wamekubaliana na ombi la Paroko wa Kakonko la kutaka marehemu Bilago ibada ya kumuaga ifanyike Kanisani lakini akaeleza Chadema imeamua Jumatano aagwe katika viwanja vya wazi na kisha siku inayoafuata(Alhamisi) ndio itakuwa kanisani.
Akizungumzia taarifa za kifo cha mbunge huyo amesema alifariki dunia Jumamosi mchana siku ya Jumamosi wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili na taarifa za kuumwa kwake alizipata akiwa nchini Afrika Kusini.Hivyo aliagiza wabunge na viongozi wengine wa Chadema kufanya jitihada za kuhakikisha anapata matibabu.
"Akiwa hospitali ya Muhimbili alinitumia ujumbe kupitia simu yangu ya mkononi akinieleza kuwa anaumwa sana na akahitaji nije kumuona.Lakini wakati ananitumia ujumbe huo sikuwepo nchini."Hivyo niliporudi nikaenda kumuona hospitali na tukawa na mpango wa kumpeleka nje kwa matibabu lakini ilipofika Jumamosi akafariki dunia,"amesema Mbowe na kuongeza Chadema imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Mbunge wao makini na ni pigo kwa familia.
Awali akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wa marehemu Bilago, Paroko wa Parokia ya Magomeni jijini Dar es Salaam Christan Nyumayo amesema enzi za uhai wake kiongozi huyo alikuwa ameweka maisha yake kwenye imani ya dini yake na hata Parokia ya Kakonko imethibitisha hilo na ndio maana inataka lazima ibada yake ikafanyike ndani ya Kanisa.
Pia amesema maisha yake aliyandaa akiwa hai na ndio maana leo hii anaagwa kwa heshima kubwa ,hivyo ametoa rai kwa walio hai kuhakikusha wanatenda mema na kuandaa maisha yao ya baadae."Ukiwa kibaka katika uhai wao kuna uwezekano mkubwa wa kuzikwa na vibaka wenzako na ukiwa mcha Mungu basi utazikwa na wacha Mungu.Hivyo tunachoshuhudia leo hii ndugu yetu amepata heshima ya kuagwa katika mazingira ya utulivu na unyenyekevu kwasababu aliishi maisha ya kumpendeza Mungu.Nilipopata taarifa za kutakiwa kuja hapa sikuwa na shaka ya aina yoyote,"amesema Paroko Nyumayo.
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ,ukiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa mapema leo mchana jijini Dar.

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema),ukiingizwa ndani ya ukumi wa Karimjee,mapema leo mchana tayari kwa kuagwa na waombolezaji mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa chama cha CHADEMA.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa chama cha CHADEMA,wakiwa ndanni ya ukumbi wa Karimjee tayari kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa bunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,tayari kwa kutokewa heshima za mwisho na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho pamoja na waombolezaji wengine.
Baadhi ya waombolezaji wakishiri sala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
Baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA na baadhi ya waombolezaji wakishiriki sala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
Baadhi ya Waandishi wa habari wakirekodi tukio la kuwasili mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .PICHA NA MICHUZIJR.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.