Habari za Punde

NGORONGORO HEROES KUWAKARIBISHA MALI MEI 12, MASHABIKI KIINGILIO BUKU VIP BUKU 3

 Ofisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu TFF, Cliford Ndimbo, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tff leo mchana.
*****************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar.
TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) inatarajia kucheza na timu ya Taifa ya Mali U20 Jumapili ya Mei 12,2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Katika mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni kiingilio cha kuingia Uwanjani kutazama mechi hiyo VIP zote itakuwa ni shilingi 3,000 na mzunguko utakuwa ni shilingi 1,000.Aidha TFF imepanga viingulio hivyo ili,  iwe rahisi kwa mashabiki wengi kujitokeza kuwashangilia vijana wao ambapo kila mmoja atamudu viwango hivyo.Ngorongoro Heroes wapo kambini wakiendelea kujiandaa na mchezo huo,leo wapo kwenye ratiba ya kufanya mazoezi ya gym asubuhi na jioni kabla ya kuwa na mazoezi ya uwanjani kesho na Ijumaa ambapo kesho Alhamisi watakuwa na kipindi kimoja cha Uwanjani saa 10 kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Ijumaa watafanya vipindi viwili asubuhi na jioni saa 10.
Ngorongoro Heroes walifanikiwa kuwaondoa timu ya vijana ya Congo Drc kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoka sare ya 1-1 hapa jijini Dar es salaam na 0-0 nchini Congo kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba.Mpaka sasa kikosi hicho hakina majeruhi vijana wana morali kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu fainali za vijana Africa, ambao utakuwa ni kwa ajili ya kufuzu kwenda katika fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.