Habari za Punde

RAIS MAGUFULI KUNOGESHA UBINGWA WA SIMBA KUWAKABIDHI KOMBE UWANJA WA TAIFA


 Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF, Wallace Karia, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za TFF, jijini Dar es Salaam, leo mchana, wakati akitangaza mgeni rasmi katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, ambapo alimtangaza Rais Dkt Magufuli ambaye atawakabidhi Kombe la mshindi wa Ligi Kuu Simba kwa msimu wa 2017-18.

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, leo amemtangaza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Kagera Sugar unaotarajia kupigwa Mei 19 mwaka huu.
Aidha amesema kuwa Shirikisho limemuomba, Dk. Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ili kuwakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, Simba SC siku hiyo katika Uwanja wa Taifa jijin Dar es Salaam.Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya ofisi za TFF, Dar es Salaam, Karia amesema mpaka sasa wanasubiri majibu kuhusu ombi hilo.
Pamoja na hayo, Rais Karia amesema kwamba siku hiyo kama Rais Magufuli atakubali mwaliko huo, ataanza kwa kukabidhiwa Kombe la ubingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (CECAFA U17), ambalo Tanzania ilitwaa mapema mwezi huu nchini Burundi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.