Habari za Punde

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA UJUMBE WA EU

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (katikati) akieleza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya kujadiliana Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na jumuiya hiyo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mkuu Mst. (Znz) Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Giveness Aswile.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (wa nne kushoto) akifafanua jambo kwa Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Roeland Van de Geer (wa pili kushoto) na Mtaalau wa Masuala ya Siasa wa EU, Anna Costantin.Ujumbe huo ulifika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam kujadili Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ilyotolewa na jumuiya hiyo.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Asina Omari (wa pili kulia) akiwasilisha taarifa fup kuhusu Tume na majukumu yake kwa ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) (kushoto) uliofika ofisi za NEC kujadili Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na jumuiya hiyo.Katikati ni Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage.Picha na Hussein Makame-NEC

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.