Habari za Punde

YANGA YASHINDWA KUTUMIA NAFASI UWANJA WA NYUMBANI YASULUHU 0-0

 Mshambuliaji wa Yanga, Yusuph Mhilu (kushoto) akiwania mpira na beki wa Rayon Sports ya Rwanda, Mutsinzi Ange, wakati wa mchezo wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho wa Kundi D, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitosa suluhu 0-0 na kuifanya Yanga kuendelea kuburuza mkia katika kundi hilo ikiwa na pointi 1 huku Rayon wakijiongezea pointi 1 na kufikisha pointi 2.
***************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar.
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi Dar Young Africans, wameshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda baada ya kulazimishwa suluhu ya 0-0.
Yanga waliokuwa dimba la nyumbani Uwanja wa Taifa walikubali matokeo hayo baada ya kushindwa kupata goli la ushindi na wazi kupitia kwa mshambuliaji wake Obrey Chirwa aliyebaki na nyavu na kugongesha mwamba wa juu katika kipindi cha pili.
Mchezo huo ulioanza majira ya saa 1 usiku Yanga waliweza kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza wakionekana kutawala sehemu ya kiungo kupitia na Thaban Kamusoko na Pius Buswita.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Kocha msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema kuwa hajaridhishwa na matokeo ya leo dhidi ya Rayon Sports kwani walihitaji ushindi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda hatua inayofuata.
"Sijaridhishwa na matokeo ya leo, katika mchezo huu tulihitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua inayofuata ila wachezaji walikosa umakini na kushindwa kutumia nafasi walizozopata,"amesema Mwandila.
Aidha Mwandila amesema kwa sasa mashindano hayo yanasimama kwa muda mpaka mwezi wa saba ambapo wao sasa wanatumia muda huo kwa ajili ya kukiunda kikosi na kukifanya marekebisho katika nafasi zinazohitajika ili waweze kufanya vizuri kwenye michezo inayofuata.
Baada ya mechi hii Yanga wanakuwa na alama 1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa huku Rayon wakiwa na alama 2.
 Mwashiuya akijikunja kupiga shuti
 Nyota wa mchezo Hassan Kessy akiambaa na mpira

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.